Mshambuliaji wa Tanzania George Mpole ameibuka mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, baada ya kufunga bao lake la 17 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Mpole alifungia timu yake ya Geita Gold bao la kuongoza katika Uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga, kabla ya wenyeji Coastal Union kusawazisha na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Mpole anakua Mshambuliaji wa Kitanzania aliyefunga mabao mengi zaidi msimu huu, akifuata nyayo za Nahodha na Mshambuliaji wa Simba SC John Bocco ambaye alimaliza kinara wa ufungaji Bora msimu uliopita kwa kufunga mabao 17.

Nafasi ya pili ya ufungaji Bora inaendelea kushikwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo na klabu ya Young Africans Fiston Mayele.

Kwa sare ya bao 1-1 Geita Gold imemaliza Msimu wa 2021/22 ikiwa nafasi ya nne kwa kufikisha alama 46, ikitanguliwa na Azam FC yenye alama 49, kufuatia ushindi wa 4-1 iliyoupata dhidi ya Biashara United Mara.

Simba SC inayoshika nafasi ya pili imefikisha alama 61, baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Mbeya Kwanza FC, iliyokua nyumbani katika Uwanja wa CCM Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Young Africans imeibanjua Mtibwa Sugar 1-0, na kuendeleza ubabe wa kukaa kileleni huku ikifikisha alama 74.

Matokeo ya michezo mingine

Ruvu Shooting 1-0 TZ Prisons

Dodoma Jiji 1-0 KMC FC

Kagera Sugar 0-0 Polisi Tanzania

Mbeya City 1-1 Namungo FC

Biashara Utd yashuka Jumla Jumla
Vigogo CWT kurejesha pesa, jela yawahusu