Beki wa kati kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Gabriel Zakuani, ameitosa klabu ya Northampton na kukubali kujiunga na klabu hasimu ya Gillingham.

Zakuani, mwenye umri wa miaka 31, kabla ya kufanya maamuzi ya kuikacha Northampton inayoshiriki ligi daraja la pili nchini England, alikuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya lakini hakuridhishwa na ofa aliyoahidiwa na viongozi wa klabu hiyo.

Beki huyo ameondoka Northampton huku  akiacha kumbukumbu ya kucheza michezo 25 msimu uliopita.

Saa kadhaa baada ya kuthibitika amejiunga na Gillingham, imefahamika kuwa, Zakuani amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo kutoka barani Afrika, anakua watatu kusajiliwa na Gillingham katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi akitanguliwa na Luke O’Neil na Alex Lacey.

ACT Wamvua Uenyekiti Anna Mghwira, Washauri Uteuzi Ufuate Taratibu Hizi
Eduardo Berizzo Kuanza Na Batshuayi