Mkurugenzi mkuu wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, Giuseppe Marotta amekanusha taarifa za kufikia makubaliano na viongozi wa klabu ya Man Utd kuhusu usajili wa kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba.

Marotta, amesema hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa hizo ambazo zimechukua nafasi kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari duniani kote kwa kuripotiwa kwamba, Man Utd wamekubali kulipa ada ya usajili ya kiungo huyo.

Ada ya usajili ya Pogba ilitangazwa na mabingwa hao kuwa ni Pauni milioni 100, na mapema hii leo vyombo vingi vya habari vya barani Ulaya vimeripoti kwamba Man Utd wamekubali kutoa kiasi hicho cha pesa ambacho ni sawa na Euro milioni 120.

“Hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika kuhusu Pogba,”

“Taarifa hizo zimekua tofauti kabisa na suala lenyewe linavyokwenda, kama kutakua na jambo lolote tutawafahamisha itakapofika siku ya ijumaa.”

Marotta alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Italia saa moja iliyopita.

Siku ya ijumaa Jose Mourinho pamoja na kikosi chake watakua nchini China kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund.

Man Utd tayari wameshawasiliha ofa ya awali ya zaidi ya Pauni milion 85, lakini ilikataliwa na viongozi wa Juventus, kwa kigezo cha kutokua na thamani sawa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.

Kufungiwa kwa Wimbo Kunamrudisha Msanii Nyuma- Shaa
Pep Guardiola: Tutamsajili Leroy Sane