Meneja wa klabu ya Man City, Pep Guardiola amethibitisha taarifa za klabu hiyo kuwa katika mazungumzo na uongozi wa klabu ya Schalke 04, kwa ajili ya kuangalia uwezkano wa kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ujerumani Leroy Sane.

Guardiola, alithibitisha ukweli wa jambo hilo usiku wa kuamkia hii leo, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Munich nchini Ujerumani, ambapo kikosi chake kilikua kinakabiliwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya FC Bayern Munich.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania, alisema anaamini mazungumzo hayo yatafikia pazuri na kufanikisha azma ya kufanya kazi na Leroy Sane katika ligi ya nchini England pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2016/17.

Alisema anaamini mchezaji huyo atakua na nafasi kubwa ya kuonyesha uwezo wake katika ligi ya nchini England, kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina ya ligi ya EPL na ile ya Ujerumani.

Katika mchezo huo wa kirafiki FC Bayern Munich walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na Erdal Oeztuerk katika dakika ya 76.

Giuseppe Marotta: Hakuna Makubaliano Yoyote Kuhusu Pogba
Leonardo Bonucci Ni Chaguo Lingine La Mourinho