Nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezman ambae amekua akihusishwa na kuhamia katika timu ya Manchester United amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuihama timu yake hiyo katika dirisha kubwa la usajili.

Griezman ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Television moja huko nchini Ufaransa, amesema kuwa uhamisho huo unawezekana kwa asilimia 6 kati ya 10 ambapo ameonyesha nia ya kujiunga na timu hiyo ya Manchester United.

“Nafikiri nitaamua kuhusu hatma yangu ndani ya wiki mbili zijazo, kwa sasa sitaweza kuongelea hili jambo lakini muda ukifika nitaongea kuhusiana na uhamisho wangu kama naenda ama nabaki na timu yangu,”amesema Griezman.

Hata hivyo, Mchezaji huyo ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa michezo 41 tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwak 2017 na amefunga jumla ya mabao 26 mismu huu akiwa na timu yake ya Atletico iliyomaliza ligi katika nafasi ya tatu

Wachapwa viboko 85 kwa kosa la kufanya mapenzi ya jinsia moja
Yanga yakanusha taarifa za kujiuzuru kwa Manji