Meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, Josep Pep Guardiola Isala amesema litakua jambo jema endapo ataendelea kufanya kazi na kiungo Bastian Schweinsteiger.

Guardiola ameelezea hayo kufuatia fununu za kuondoka kwa Schweinsteiger kuendelea kupewa nafasi kubwa, baada ya mkurugenzi wa michezo wa The Bavarians, Matthias Sammer kusema kiungo huyo huenda akaondoka katika kipindi hiki cha usajili.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amesema anafurahishwa na uwajibikaji wa Schweinsteiger, huku akiahidi kufanya nae mazungumzo, kwa kumshawishi abaki klabuni hapo.
Hata hivyo Guardiola, amesema kama itashindikana ataheshimu maamuzi yatakayochukuliwa na Schweinsteiger.

Tayari kituo cha televisheni cha Sky cha nchini England kimeshaeleza kwamba jina la Schweinsteiger, ni miongoni mwa majina ya wachezaji ambao wanahitajika huko Old Trafford yalipo makao makuu ya klabu ya Man Utd.

Schweinsteiger, yupo katika mikakati ya kutaka kuondoka nchini Ujerumani, baada ya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na viongozi wa klabu ya Bayern Munich kusua sua huku mkataba wake wa sasa ukisaliwa na muda wa mwaka mmoja.

Song Ajitabiria Maisha Ya Kudumu Magharibi Mwa London
Muhanga Wa Tsunami Asajiliwa Sporting Lisbon