Wagonga nyundo wa jijini London, wanakaribia kusajili moja kwa moja kiungo kutoka nchini Cameroon, Alexandre Dimitri Song, baada ya kumtumikisha kwa mkopo msimu uliopita akitoka kwa mabingwa wa soka barani Ulaya, FC Barcelona.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni cha Sky cha nchini Uingereza, imebainika kuwa viongozi wa klabu ya West Ham Utd wapo katika mazungumzo na viongozi wa Barca kwa ajili ya kukamilisha mkakati huo.

Kubwa lililowapa jukumu viongozi wa The Hammers kukaa meza moja na viongozi wa klabu bingwa nchini Hispania ni kuridhishwa na kiwango cha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

Hata hivyo, tayari Song ameshaonyesha matarajio ya kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha West Ham Utd, baada ya kuthibisha jambo hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa kuweka picha inayomuonyesha akiwa Gym akifanya mazoezi huku akiwa amevalia mavazi ya The Hammers.

Kimtazamo, Song kwa sasa hana nafasi kubwa ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha Barcelona kutokana na umahiri ulioonyeshwa na wachezaji aliowaacha klabuni hapo msimu uliopita, hivyo iwe isiwe ni lazima atauzwa.

Bilic Aanza Kazi Kwa Mbwembwe Upton Park
Guardiola Aanza Kujipendekeza Kwa Schweinsteiger