Meneja mpya wa klabu ya West Ham Utd, Slaven Bilic ameanza vyema kibarua huko Upton Park baada ya kukishuhudia kikosi chake kikifanya kweli usiku wa kuamkia hii leo katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya Europa League msimu wa 2015-16.

West Ham, wamepangiwa kuchezo na FC Lusitans ya nchini Ureno, na tayari imeshajiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kufuatia ushindi wa mabao matatu kwa sifuri waliouvuna kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Mshambuliaji kutoka nchini Senegal, Diafra Sakho alifanya shughuli ya kuwaridhisha mashabiki wa West Ham Utd chini ya meneja wao mpya Slaven Bilic, kwa kufunga mabao mawili katika dakika ya 40 na 45 huku beki wa kati kutoka nchini England James Oliver Charles Tomkins akifunga bao la tatu katika dakika ya 58.

Mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya Europa League kati ya West Ham Utd dhidi ya FC Lusitans utaungruma nchini Ureno juma lijalo.

Bilic amepewa jukumu la kukiongoza kikosi cha West Ham Utd ambacho aliwahi kukitumikia kama mchezaji kuanzia mwaka 1996–1997, baada ya kuondoka kwa Samuel “Sam” Allardyce “Big Sam”

Michuano Ya Wimbledon, Nadal Atupwa Nje
Song Ajitabiria Maisha Ya Kudumu Magharibi Mwa London