Klabu ya Man City huenda ikakubali kumuachia kiungo mshambuliaji kutoka nchini Hispania David Silva kwa makubaliano ya kumsajili kinda wa klabu ya Borussia Dortmund Julian Weigl.

Tovuti ya Calciomercato imechapisha taarifa za kuwepo kwa uwezekano huo kufuatia meneja wa Man City Pep Guardiola, kuonyesha anamuhitaji kinda huyo mwenye umri wa miaka 21.

Silva amekua kiungo muhimu katika kikosi cha Man City tangu aliposajiliwa mwaka 2010, lakini katika mipango ya Guardiola ameonekana kutokua na umuhimu wowote, na ndio maana anafikiriwa kuingizwa katika dili hilo.

Taarifa za tovuti hiyo zimesisitiza kuwa, tayari Guardiola ameshawasilisha pendekezo la kukubali kumuachia Silva, ili afanikishe azma ya kusajiliwa kwa Weigl ambaye ni raia wa nchini Hispania.

Guardiola amekua na mapenzi na Weigl tangu akiwa nchini Ujerumani alipokua akikinoa kikosi cha FC Bayern Munich, na mara kadhaa alipendekeza asajiliwa na mabingwa hao wa Bundesliga, lakini itikadi za ushindani dhidi ya Borussia Dortmund zilikwamisha mpango huo.

Mabadiliko Ya Simba SC, Yanga SC Yapigwa Stop
Laurent Blanc Kuchukua Nafasi Ya Frank De Boer?