Meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, Josep Pep Guardiola amethibitisha kutarajia upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wake Arsenal katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa usiku wa leo.

Guardiola, amethibitisha jambo hilo, kwa kutambua umuhimu wa mchezo wa hii leo, ambapo anatambua wazi Arsenal watahitaji kucheza kwa nguvu ili kujitengenezea mazingira ya ushindi ambao utawaweka salama kwenye msimamo wa kundi la sita.

Amesema jambo hilo ameshalitambua tangu alipoanza safari ya kuelekea nchini England mwishoni mwa juma lililopita, hivyo amekiandaa kikosi chake kukabiliana na uzito wa mchezo huo, ambao utachezwa kwenye uwanja wa Emirates huko kaskazini mwa jijini London.

Tayari FC Bayern Munich, wameshajinyakulia point sita katika msimamo wa kundi la sita, baada ya kushinda michezo ya mizunguuko miwili iliyopita dhidi ya Dynamo Zagreb pamoja na Olympiakos.

Kwa misimu mitatu sasa Arsenal wamekua wakikutana na FC Bayern Munich kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambapo katika michezo ya msimu wa 2012-13, The Guners  wakicheza nyumbani walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri, na katika mchezo wa mkondo wa pili The Gunners walipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Msimu uliofuata wa 2014-15 Arsenal walikubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri kwenye uwanja wao wa nyumbani na walipokwenda mjini Munich walilazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

 

Djibril Cisse Atangaza Kustaafu Soka
Kiiza Mchezaji Bora Mwezi Septemba