Aliyekua mshambuliaji wa klabu za Liverpool, Sunderland pamoja na Queens Park Rangers zote za nchini England, Djibril Cisse, ametangaza kustaafu soka.

Cisse mwenye umri wa miaka 34, alitangaza uamuazi huo usiku wa kuamkia hii leo kupitia kipindi maalum kilichoandaliwa na kituo cha televisheni huko nchini kwoa Ufaransa.

Cisse alitangaza uamuzi huo, na kisha alimwaga machozi kutokana na hisia zake kumtuma huenda kuna jambo litakosekana kutoka kwake ama kwa mashabiki ambao siku zote wamekua wakimfuatilia anapokua uwanjani.

Amesema sababu kubwa iliyopelekea kujiweka pembeni na mchezo wa soka, ni kuhitaji kuwapisha wengine ili waweze kuonekana, baada ya yeye kuwa sehemu kubwa ya wachezaji waliowahi kutamba akiwa na klabu kadhaa za barani Ulaya pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa.

Cisse, ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake alioutoa kwenye timu ya taifa lake la Ufaransa kwa kucheza michezo 45 na kufunga mabao 15, huku akicheza soka kwenye klabu 12.

Katika mizunguuko ya kucheza soka lake upande wa klabu, Cisse, alibahatika kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kilichotwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2004-05.

Akiwa kwenye klabu ya Liverpool alicheza michezo 49 na kufunga mabao 24.

Klabu nyingine alizowahi kuzitumikia ni Olimpic Marseille, Panathinaikos, Lazio, Sunderland, Queens Park Rangers, Al-Gharafa, Kuban Krasnodar, Saint-Pierroise, Bastia, Sunderland pamoja na Auxerre.

Kwa ujumla Cisse amefunga mabao 250 katika klabu zote alichezocheza.

Amuweka Rehani Mkewe Kisa Lowassa, Magufuli
Guardiola: Ninajua Ugumu Wa Game Ya Leo