Harakati za uchaguzi mkuu wa mwaka huu zitaacha historia kubwa sio tu katika ngazi ya kitaifa lakini hata katika ngazi za mtaa ambapo mengi yasiyo ya kawaida yameonekana kufanywa na wafuasi wa vyama vya siasa wanaoamini mgombea wao atashinda kwa kishindo.

Katika hali isiyotegemewa, mkazi mmoja wa Mtaa wa Bendera ya CUF jijini Dar es Saalam, Martine Mkude ambaye ni mfuasi wa CCM amemuweka rehani mkewe akimuahidi mfuasi wa Chadema aliyekuwa anabishana naye, Juma Hassan kuwa endapo Edward Lowassa atashinda na kuwa rais wa Tanzania basi atampa mkewe amuoe kwa mara ya pili.

“Haki ya Mungu..! kama Lowassa akiwa Rais basi mimi nitakupa mke wangu umuoe upya,” alisema Juma Hassan baada ya mabishano ya muda mrefu yaliyokusanya watu wengi katika eneo hilo kusikiliza.

Ingawa wengi walidhani Martine anatania, Juma Hassan alimtaka mpinzani wake huyo kuihakikisha ahadi yake kwa kumuandikia kwa maandishi mbele ya balozi wa nyumba kumi ili itakapotokea asikatae.

Mashuhuda wa tukio hilo walinogesha ubishani huo na kuchangia kalamu na karatasi kisha kumuita Mjumbe wa Nyumba Kumi, Hassan Mbwita baada ya mtoa ahadi kusisitiza kuwa hafanyi utani katika hilo.

“Mimi Martine Mkude, nitakuwa tayari kumwachia mke wangu Rehema Mkude awe mke wa Juma Hassan endapo Lowassa atashinda urais mwaka huu,” yalisomeka maandishi yaliyotiwa sahihi.

Shukurani za pekee ziende kwa mwandishi wa Mwananchi aliyeshuhudia na kuripoti tukio hili lenye ucheshi na kushangaza.

Ushabiki huu utavunja ndoa …!

 

Ratiba Ya Mzunguuko Wa 11 Yapanguliwa
Djibril Cisse Atangaza Kustaafu Soka