Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Uingereza ziara ambayo anaifanya wakati taifa hilo likijaribu kupata ushirikiano wa umoja wa Ulaya kuhusu mpango wake wa kujitoa BREXIT.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza na Marekani vimeripoti kuwa ziara hiyo imezua gumzo baada ya matamshi ya Rais Trump ya hivi karibuni ambyo alisema wazi kuwa anamuunga mkono kiongozi wa upinzani Nigel Farage na kwamba angepaswa kujumuishwa kwenye mazungumzo ya BREXIT.
Kabla ya kuwasili London kutoka washington DC kulikuwa na fununu kuwa wanaharakati wamepanga kufanya maandamano makubwa jijini Londoni na miji mingine mikubwa Uingereza kupinga ziara hiyo.
Kwenye mahojiano na gazeti la The Sun mbali na kumuunga mkono Farage, Raisi Trump amesema kuwa angependela kuona Boris Johnson anateuliwa kuwa waziri mkuu ajae.
Hata hivyo Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri mkuu mpya hivi kribuni baada ya Theresa May kutangaza kuwa atajiuzulu juni 7 mwaka huu.
Mara baad ya kuwasili jijini Londoni taarifa zilisema kuwa Rais Trump aliandaliwa dhifa malumu na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ambapo ameambatana na mke wake Melania Trump.
- Serikali ya Kenya yaitangaza siku ya Eid al Fitr
-
Marekani kuchunguza taarifa za mitandao ya kijamii za wanaoomba VISA
-
MacLeans BeneCIBO yatua Lushoto mkoani Tanga kwa Mkulima