Aliyekua meneja wa klabu ya Sunderland, Gus Poyet ametangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu ya AEK Athens ya nchini Ugiriki.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 46, ametangazwa kuchukua ajira hiyo, baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa AEK Athens sambamba na kusaini mkataba utakaofikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Poyet, aliwasili mjini Athens, siku ya jumatano kufuatia wito alioupokea kutoka kwa viongozi wa klabu ya AEK Athens, ambao tayari walikua wamechukua maamuzi ya kumtimua aliyekua meneja klabuni hapo Traianos Dellas, baada ya kikosi chake kukubali kufungwa mabao manne kwa sifuri dhidi ya vinara wa ligi ya nchini Ugiriki, Olympiakos Piraeus.

Hii leo, Poyet anatarajia kutambulishwa kwa waandishi wa habari na uongozi wa klabu ya AEK Athens, huku jukumu kubwa lililo mbele yake ni kuisaidia klabu hiyo kufikia malengo yanayokusudiwa kwa msimu huu.

AEK Athens, kwa sasa ipo kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, kwa tofauti ya point nane dhidi ya vinara wa ligi ya nchini Ugiriki Olympiakos wenye point 24.

Scholes Ampa Makavu Live Louis Van Gaal
Malinzi Ampongeza John Pombe Magufuli