Lydia Molell, Kilosa – Morogoro.
Zaidi ya Kaya 100 zimekosa makazi baada ya Nyumba zao kusombwa na kubomolewa na Maji, kufuatia Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Desemba 10, 2023 ambazo pia zimeharibu madaraja manne Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewapa pole waathiriwa huku akiwataka kuacha kujenga katika maeneo ambayo Mkondo wa maji unapita, ili kuepuka adha zinazosababishwa na maafuriko.
Hata hivyo, Wananchi wamejibu kwa kusema hawajajenga katika mkondo wa Maji bali ujenzi wa Daraja la Mwendokasi umesababisha Maji kukosa muelekeo na kuingia katika makazi yao na zifuatazo ni Picha zikionesha baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa katika Wilaya hiyo.