Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Makamu wake Dkt. Philip Mpango kutoumizwa na naneno mabaya ya mitandaoni juu yake, ikiwemo kumzushia kifo, kwani wazushi huwa hawakosekani.

Dkt. Samia  ameyasema hayo hii leo Desemba 10, 2023 katika hafla  ya kupokea hundi ya mchango wa maafa yaliyotokea mji wa Katesh Wilayani Hanang’ iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amesema, “Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Isdory Philip Mpango karibu nyumbani, karibu nyumbani na nikwambie tu ukiwa Kiongozi wewe ni puplic figure.”

Dkt. Samia ameongeza kuwa, “Sasa kuna wale watakaojiuliza sasa kwa kweli yupo wapi mbona hatumuoni,lakini kuna wazushi tu wanaoamua kuzusha na kuleta taharuki kwenye nchi, sasa sisi Viongozi tuyapokee tu lakini karibu Nyumbani kama ulivotukuta tunashukuru umerudi unaungana nasi.”

Mvua zasababisha zaidi ya Kaya 100 kukosa makazi Kilosa
Madawati ya jinsia tunzeni siri