Klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara amesema TFF kuendelea kufumbia macho kauli za kejeli, dharau, matusi na kashfa zitolewazo na afisa habari wa klabu ya Yanga kutawafanya wao wachukue hatua.

Manara amesema wakati alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akidai klabu ya Simba imechoshwa na kauli za Muro huku TFF ikiendelea kubaki kimya.

“Mwishoni mwa mwaka jana msemaji wa Yanga akiwa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, aliidhihaki klabu ya Simba na viongozi wake kwa lugha za kashfa, kejeli, dharau na matusi. Alifikia mahali anamwita makamu wa klabu ya Simba sanamu la michelini, mbaya zaidi alinikashfu binafsi lakini kubwa alilikashfu kabila la Wazaramo”.

“TFF ikatoa kauli kwamba mwanzoni mwa mwaka huu (January) itamchukulia hatua za kinidhamu kutokna na kauli zile, January imepita, February inamalizika. Hatukusema kitu, baada ya mechi ya juzi mmesikia kashfa zake na maneno yake”.

Jerry Muro

“TFF wako kimya, kesho Simba tukianza kusema maneno ya kihuni watatuhukumu? Hayo mamlaka yatatoka wapi? Kama wanashindwa kuchukua hatua kwa mtu anayetudhalilisha kila kukicha anajenga chuki na uhasama”.

“Angalieni records, kamtukana mtu wa bodi ya ligi, kamtukana makamu wa rais wa Simba, kamtukana Haji Manara, kaitukana ile timu ya Kimondo, kila siku anatukana tu. TFF wasipochukua hatua Simba tutachukua hatua sitishi litakalotokea tusilaumiane”.

TMF yajitolea kulipa gharama za Bunge Kurushwa ‘Live’ TBC1
TANZIA: Kassim Mapili Afariki Dunia