Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara jana alipata ajali mbaya.

Manara alipata ajali hiyo baada ya kuchomoka akitokea ndani ya Bajaj na kuanguka barabarani.

Kuanguka huko kulimsababishia Manara kupata majeraha sehemu za mkononi na usoni huku akisema amenusurika kifo kutokana na ajali hiyo.

“Nilikuwa nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj.

Sasa tukio hilo limetokea hivi, Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa sijashika, ndiyo nikachomoka.

“Hakika nimeumia na nina maumivu makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.”  Manara alieelezea tukio hilo

 

Ronaldo, Messi Watuhumiwa Kumbana Neymar
Kocha Mayanja Amfukuza Kambini Hamisi Kiiza