Hali imeendelea kuwa tete Wilayani Kibiti Mkoani Pwani mara baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na kufariki usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana, kisha kutokomea kusikojulikana.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi amesema kuwa ni kweli mtu mmoja amefariki na taratibu za upelelezi za kuwabaini waliohusika katika tukio hilo zinaendelea.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa zilizopo zimesema kuwa mtu huyo aliyeuawa ni kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne wilayani Kibiti.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Dar es salaam amethibitisha kutokea mauaji hayo ingawa hakutaka kuweka wazi aliyeuwawa ni nani na kusema wakifika eneo la tukio ndipo watajua ni nani aliyefariki na kutoka taarifa rasmi.

Wamiliki wa shule binafsi na waandishi wa habari 10 watiwa mbaroni Jijini Arusha
Kaburu: Yanga wanashangilia ubingwa hewa