Halmashauri Nchini zimeombwa kujifunza namna ujenzi wa mradi wa soko kuu la Njombe unavyojengwa ili kuendana na ujenzi wa majengo yenye viwango.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Tamisemi, Joseph Kandege wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko kuu la Njombe Mjini.

“Miongono mwa masoko ambayo yanajengwa kwa ustadi mkubwa ni pamoja na hili soko la Njombe TC kwanza nawapongeza kwa kuchagua mradi huu na uhakika mradi ukikamilika kwa kiwango wanachotarajia itakuwa ni miongoni mwa Miradi mizuri kabisa, halmashauri zingine waje kujifunza katika mradi huu,”amesema Kandege

Aidha, ameongeza kuwa Ramani hiyo ameridhika nayo kwakuwa ni ramani ya soko la kisasa na likikamilika litakuwa ni miongoni mwa masoko ya kisasa katika halmashauri na amempongeza mkurugenzi na timu yake, wilaya na mkoa.

Hata hivyo, Soko hilo linaloghalimu zaidi ya bilioni saba linategemewa kukamilika mwezi wa sita mwaka huu na kuanza kuwanufaisha zaidi ya wafanyabiashara 1000 mjini Njombe.

Video: Chege atoboa siri kumfukuzia Vanessa miaka mitatu
Uingereza yatahadharisha uwezekano wa kutokea vita ya Nyuklia Duniani

Comments

comments