Manispaa na Halmashauri nchini zimetakiwa kuongeza kasi katika ukusanyaji kodi ya ardhi na Nyumba ili kuweza kuongeza kasi na tija ya maendeleao ya sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Wziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula katika ziara yake ya siku mbili kwa Manispaa za Kinondoni, Temeke na Ilala, ambapo amesema kuwa sekta ya ardhi katika Manispaa na halmashauri mbalimbali nchini itajiendesha kwa ukusanyaji kodi kwa pango la ardhi.

Amesema kuwa ukusanyaji kodi kwa njia ya mfumo mpya uliofungwa kwenye Manispaa ni njia bora ya kupata mapato na kuendeleza sekta ya ardhi, kwa hiyo watumishi wa idara hiyo waweke juhudi za kudai kodi hiyo hasa kwa wadaiwa sugu.

“Katika mfumo huu wa kodi na nimeona baadhi ya takwimu kwa wateja wanaodaiwa, kati ya wateja 35,000 nimechukua wateja 100 wanaodaiwa kuanzia 5,000,000 na jumla yao ni  bilioni 13 kwa hiyo tukiweza kuwadai tutapata fedha nyingi tu,” amesema Mabula.

Aidha, amesema kuwa juhudi za ukusanyaji kodi zimerahisishwa kwani mfumo huo mpya utawawezesha watumishi katika idara ya ardhi kupata takwimu kwa urahisi na kuweza kupata majina ya wadaiwa sugu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Maafisa ardhi hawana budi kutumia mfumo huo mpya kwa kuwa hauhitaji muda mwingi kutafuta taarifa katika mafaili yaliyopo masijala kwa ajili ya kukagua takwimu na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha makusanyo ya kodi ya ardhi.

 

Nchemba awataka wananchi kushirikiana
Umoja wa Ulaya wagoma kuisaidia Hispania