Mshambuliaji mahiri wa klabu Tottenham Hotspurs, Harry Kane amekanusha uvumi wa kutaka kuikacha klabu hiyo na kuelekea mjini Madrid nchini Hispania kujiunga na klabu nguli ya Real Madrid.

Kane, amevunja ukimya wa suala hilo, kufuatia taarifa kuendelea kutoka kila kukicha ambapo inadaiwa uongozi wa klabu ya Real Madrid umejiandaa kumsajili.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema haoni sababu ya kuondoka kwa sasa huko White Hart Lane, kutokana na imani yake kumtuma kwamba, bado ana nafasi kubwa ya kusaka mafanikio akiwa jijini London.

Amewataka mashabiki wake kutambua kwamba, katika kipindi hiki yapo mengi watakayoendelea kuyasikia kupitia vyombo vya habari, lakini ukweli anaujua yeye kama muhusika wa jambo hilo.

Kane amekua katika harakati za kuhusishwa na taratibu za usajili tangu alipoanza kuonyesha makali katika safu ya usahambuliaji ya Spurs misimu miwili iliyopita.

Klabu nyingine ambayo imekua ikitajwa katika hatua za kumuwania Harry Kane, ni Man Utd inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Video: Beka afunika na Cover ya 'Hello' japo hajui Kabisa Kiingereza, Hutaamini
Orodha Ya Kikosi Bora Cha 2015 Yavuja