Mwimbaji hit song ya ‘Natumaini’, Beka Ibrozama ameudhihirishia ulimwengu kuwa muziki unaongea lugha ya ulimwengu mzima bila kujali kama mwimbaji anajua lugha anayoitumia.

Mkali huyo amefunika Afrika Mashariki kwa wote waliowahi kuufanyia Cover wimbo wa Adelle ambao hivi sasa umekuwa kama wimbo wa dunia uliovunja rekodi zote za mauzo ‘Hello’.

Kwa mujibu wa Beka ambaye kumbukumbu zinaoesha kuwa alishindwa kufanya mtihani wake wa mwisho wa kidato cha nne, hajui kabisa kuongea kiingereza lakini ameweza kuimba vizuri kwa lugha hiyo.

'Maalim Seif Sio Chama Cha Wananchi CUF'
Harry Kane Aikana Real Madrid