Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu na Maadili ya TFF ilitangaza kumfungia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga, Jerry Cornel Muro kujishughulisha na masuala ya soka nchini kwa mwaka mmoja kutokana na kile kinachodaiwa kutoa kauli zisizo na nidhamu kwa shirikikisho hilo.
Hata hivyo, baada ya taarifa hiyo kumfikia Muro ambaye alikuwa mapumzikoni mjini Moshi alisema angepambana nao punde tu atakaporejea jijini Dar es Salaa huku akiahidi kutokubali kukaa kando akidai kuwa yeye sio mwajiriwa wa TFF wala mwanachama wa shirikisho hilo.
Lakini leo hii kupitia akaunti yake ya Instagram, Muro ameandika maneno yenye kuashrikia kunyanyua mikono juu na kukubali adhabu hiyo ya kifungo aliyopewa.
“Kila nikizifikiria figisu za soka la bonge aisee nachoka kabisaa, let me walk away for a while though I will be missing my funs and my people wa kimataifa but I must walk away for a while @yangasc,” ameandika Jerry Muro.

Afanya ‘Honeymoon’ peke yake bila mume, kisa…
Video: Samia, Majaliwa Wawafunda Wakurugenzi