Mwili wa aliyekuwa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Hayati Patrick Mfugale utazikwa  Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda mkoani Iringa.

Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa Mfugale unatarajiwa kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam Alhamisi Julai Mosi, 2021 ukitokea Dodoma na kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo.

Ijumaa Julai 2, 2021 mwili utatolewa hospitali ya Lugalo na kupelekwa viwanja vya Karimjee ambapo wafanyakazi wa Tanroads na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi watatoa heshima zao za mwisho kisha utapelekwa Kimara Temboni nyumbani kwake.

Mara baada ya misa takatifu yaa kuuombea mwili wa mpendwa wetu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 mwili wa Mfugale utasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa ambapo unatarajiwa kuwasili Julai 4 na maziko yatafanyika Julai  5, 2021.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 1, 2021
Tanzania,Ufaransa kushirikiana uhifadhi mazingira