Mwimbaji nguli raia wa ingereza, Adele amevunja rekodi nyingine ya mauzo kupitia wimbo wake mpya ‘Hello’ uliomrudisha kwenye game kwa kishindo kufuatia mapumziko ya miaka minne.

Hello imevunja rekodi ya mauzo kwa njia ya mtandao/kidijitali baada ya kupata ‘downloads’ zaidi ya Milioni 1.1 katika wiki yake ya kwanza, kiwango ambacho hakikuwahi kufikiwa na msanii yeyote duniani.

Adele pia amemfunika Justin Bieber ambaye wimbo wake wa ‘Sorry’ ulipata kupakuliwa kwa zaidi ya mara 276,800 katika wiki yake ya kwanza.

Wimbo wa ‘Hello’ umepata mapokezi makubwa na mafanikio ya nguvu ukiwa unafungua vizuri pazia la albam mpya ya mwimbaji huyo iliyopewa jina la ‘25’.

‘25’ inafuatia albam yake aliyoitoa miaka kadhaa iliyopita ya ‘21’ iliyopata nafasi ya kushinda tuzo za Grammy na kuuza zaidi ya nakala milioni 30 duniani kote.

T.B Joshua Amebeba Ujumbe Muhimu Kwa Magufuli na Lowassa
Jeshi la Polisi Lajitoa Maandamano Ya Bila Kikomo Ya Chadema