Beki kutoka DR CongoHenock Inonga ametabiriwa kufanya mambo makubwa akiwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, baada ya kukamilisha usajili wake akitokea DC Motema Pembe.

Henonga anayecheza nafasiya ulinzi wa kati (Beki) alikua sehemu ya kikosi cha Simba kilichoweka kambi nchini Morocco, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Sifa kwa Beki huyo ambaye huitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha DR Congo, zimetolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Crescentius Magori ambapo amesema hana mashaka na uwezo wa Henonga.

“Usajili ambao umefanyika msimu huu kwa kiasi kikubwa umezingatia mahitaji ya benchi la ufundi, wachezaji wengi ambao tumewasajili umri wao ni mdogo hivyo ni faida kubwa kwenye kikosi chetu kwa misimu mingi.”

“Miongoni mwa wachezaji ambao tumewasajili ni beki Henock Inonga ambaye tumemtoa DC Motema Pembe, sina shaka juu ya uwezo wake na nina imani atafanya makubwa ndani ya kikosi cha Simba msimu huu.” amesema Magori

Henonga alikua sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichocheza michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki nchini Morocco, na alionyesha kiwango kizuri.

Jimbo la Kawe kuneemeka na mradi wa maji
Rais Samia atoa dola 100,000