Meneja wa muda wa klabu ya Chelsea, Guus Hiddink amesistiza kuwa milango bado ipo wazi kwa nahodha na beki wa kikosi chake John Terry, kusaini mkataba mpya huko Stamford Bridge.

Mwishoni mwa juma lililopita, John Terry aliweka hadharani kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu huu, pindi mkataba wake utakapofikia ikikomo, huku akidai klabu hiyo imekataa kumuongezea mkataba mpya.

Habari hizo zilipokelewa kwa mshangao mkubwa na viongozi wa klabu ya Chelsea, ambapo walidai jambo hilo halikua sahihi, na huenda lilitokana na hofu iliyokua imetanda kwa beki huyo.

Hiddink, alikuwa na maongezi ya kina na Terry mwanzoni mwa juma hili, na alipokutana na waandishi wa habari alisema beki huyo bado ana nafasi ya kuendelea kusakata soka lake Chelsea.

Amir Khan Kurejea Ulingoni Mwezi May
BEN POL, PETER MSECHU WAwazawadia mashabiki wao ‘NYOTA YA SAMBOIRA’ kuing'arisha Valentine