Waimbaji mahiri wa muziki kutoka Tanzania, Ben Pol na Peter Msechu wameachia ‘mash-up collaboration’ ya hatari, ‘NYOTA YA SAMBOIRA’ kama zawadi ya msimu huu wa Valentine kwa mashabiki wao wa dhati.

Samboila2

‘NYOTA YA SAMBOIRA’ ni muungano wa nyimbo mbili, ‘NYOTA’ ya Peter Msechu pamoja na ‘SAMBOIRA’ ya Ben Pol zilizoweka historia kwa kila mmoja kwa kufanya vizuri kipindi zilipotoka.

Kuhusu mash-up hii Ben amesema, “Katika msimu huu wa Valentines, mimi na Msechu tumeona tuwaunganishe mashabiki wetu wawe kitu kimoja kama ishara ya upendo, kwa kuwaletea Nyota ya Samboira ambayo ni muunganiko wa kazi zetu mbili zilizofanya vizuri. Hivyo ni matumaini yetu kwamba wataendelea kusambaza upendo kwa wawapendao kupitia zawadi  hii.

SABABU ZA KUREKODI MASH-UP HII:

Moja ya sababu zilizochangia wimbo huu (mash-up) urekodiwe,  kwanza ni kutokana na Ben Pol na Peter Msechu kuwa marafiki na kila mmoja kuwa shabiki wa mwenzie. Ndio maana katika ‘NYOTA YA SAMBOIRA’, Ben ameimba verse ya Msechu na Msechu ameimba verse ya Ben za kwenye nyimbo zao halisi.

 JINSI MASH-UP HII ILIVYOPATIKANA:

Mradi wa mash-up hii ulianza kama utani.

Ben na Peter walikutana kwenye studio ya Downvillah Records ambapo kila mmoja alienda kwa ratiba yake binafsi ya kurekodi nyimbo tofauti, lakini kama ujuavyo wasanii wanapokutana studio huwa panakuwa na uwezekano mkubwa  wa kufanya kitu. Hivyo wakaamua kufanya kazi lakini kwa kurudia nyimbo zao kwa mtindo wa mash-up ambayo imesimamiwa na producer Teaz Villah.

KUHUSU NYIMBO HALISI ZA ‘NYOTA’ NA ‘SAMBOIRA’

‘Samboira’ ni moja ya hits za Ben Pol iliyotoka mwaka 2011 na inayopatikana kwenye album yake ya kwanza ‘MABOMA’.

‘NYOTA’ ni wimbo wa Peter Msechu uliofanya vizuri sana mwaka jana (2015) ambao uliachiwa mwaka 2014 mwishoni.

Samboira pia ni jina la msichana aliyeimbwa kwenye wimbo wa Ben, huku Nyota ni kama ilivyo maana halisi ya nyota ing’aayo angani.

*Maelezo yametolewa na menejimenti ya wakali hao wa Bongo Fleva. Usikilize hapa:

Hiddink: John Terry Bado Ana Nafasi Ya Kuchagua
Kanye West, Wiz Khalifa wafunika kombe la bifu, Amber Rose na Kim K wakutana