Kanye West na Wiz Khalifa wameweka pembeni bifu kali lililowasha moto kwenye mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni.

Jana, Kanye West alitweet ujumbe unaoonesha kuwa yeye na Wiz walizungumza na kumaliza tofauti zao kwa amani.

Kabla ya tweet hiyo, Amber Rose ambaye pia alirusha makombora kwa Kanye West na Kim Kardashian, aliweka picha inayomuonesha akiwa na Kim Kardashian. Taarifa zilizotolewa baadae zimeeleza kuwa warembo hao walikutana na kuondoa tofauti zao.

Ikumbukwe kuwa Amber Rose aliwahi kuwa uhusiano wa kimapenzi na rappers hao kwa nyakati tofauti.

Amber Rose, Kanye

Baada ya tweet ya Kanye West, rapa Wiz Khalifa alifanya mahojiano na Angie Martinez wa kituo cha radio cha Power 105.1.

Angie alitaka kufahamu kama Wiz Khalifa alikuwa surprised kuona tweet ya Kanye West na mambo yalivyokuwa kwa upande wake.

“Nadhani kila mmoja alikuwa [surprised] lakini iko poa, tuliongea na kila kitu kiko poa,” Wiz Khalifa alieleza.

 

BEN POL, PETER MSECHU WAwazawadia mashabiki wao ‘NYOTA YA SAMBOIRA’ kuing'arisha Valentine
Dk. Slaa ajibu taarifa za nyumba yake kupigwa mnada kisa Mkewe alichukua mkopo na kumpa mwanaume mwingine