Siku chache baada ya kutoka Macca alikoenda kufanya Hijja ambayo ni moja kati ya nguvu za imani ya dini yake, muigizaji mkongwe King Majuto ametangaza mabadiliko katika uigizaji wake.

Majuto ameeleza kuwa Hijja imembadili na hivi sasa hatakuwa anaigiza filamu zinazohusisha mambo yasiyompendeza Mungu ikiwa ni pamoja na kunywa pombe.

“Sasa hivi filamu kama za kunywa pombe au kuna matukio ya kumchukiza Mungu siwezi kufanya,” Majuto ameuambia mtandao wa Bongo5.

Hata hivyo, amefafanua kuwa ataendelea kuigiza filamu ambazo hazitakuwa na matukio kama hayo kwa kuwa anataka kuwafundisha watu kufanya mambo mema.

Oscar Pistorius Atoka Jela
Sababu Za Rais Kutovunja Baraza La Mawaziri Hadi Sasa Zawekwa Wazi