Mwanariadha maarufu mlemavu wa miguu, Oscar Pistorius ametoka jela akiwa ametumikia muda wa miezi 12 kati ya miaka 5 ya kifungo alichohukumiwa kwa kumuua mpenzi wake Reeva SteenKamp.

Hivi sasa Pistorius atakuwa chini ya ulinzi katika jumba la mjomba wake ambapo ataruhusiwa kukutana na wazazi wa SteenKamp ikiwa wataridhia kukutana naye.

Wazazi wa SteenKamp wamekata rufaa wakipinga maamuzi ya mahakama hususan uamuzi wa kumuachia mapema kabla ya muda aliotakiwa kutumikia jela.

Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao (Februari 14 mwaka 2014).

 

Kiiza Mchezaji Bora Mwezi Septemba
Hijja Yambadili King Majuto, Sasa Filamu Hizi Basi