Mapema leo Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alifika Kituo cha Kati cha Polisi jijini Dar es Salaam kama alivyotakiwa na Jeshi Polisi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kuhojiwa na kuachiwa, Zitto Kabwe amesema Jeshi la Polisi linamtuhumu kufanya makosa yafuatayo :

1) maombi ya ACT ya mkutano ilikuwa ‘kujenga chama’ lakini ACT ilizindua operesheni linda demokrasia
2) kusema Rais ameropoka kuhusu sakata la sukari
3) kumchonganisha Rais na wananchi kuhusu suala la vilaza
4) kumgombanisha Rais na wananchi kwa kusema yeye anajifanya Rais wa masikini na hivyo kumgombanisha na wasio masikini
5) kumwita Rais dikteta na kwamba anaendesha nchi kwa imla.

Makosa yote hayo yako chini ya kufungu 89(1)(a) cha Penal Code ” kinachohusu kutumia maneno ya matusi yenye kuweza kuvunja amani (abusive language).

Jela miaka mitatu kwa kumtukana Rais
54 wamefikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya barabara ya mwendokasi