Jumla ya maderva 54 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya barabara ya mabasi yaendayo kasi kuanzia juni 01 hadi juni sita mwaka huu huku madereva wawili wakiwa wamehukumiwa miezi 06 jela.

Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani Mohammed R. Mpinga amesema kwamba pamoja na barabara maalumu kujengwa kwa matumizi ya magari yaendayo kasi  baadhi ya madereva wamekuwa wakipita katika barabara hizo na kusababisha ajali kwa kuyagonga mabasi  hayo ya mwendokasi.

Akizungumza na wanahabari kamanda Mpinga amesema kuwa tangu mabasi hayo kuanza kutoa huduma tarehe 10/05/2016 hadi 06/06/2016 jumla ya ajali kumi na nne zimetokea zikihusisha mabasi ya mwendokasi na magari binafsi pikipiki na bajaji.

Ameongeza kuwa kati ya ajali hizo 09 zinahusisha mkoa wa kipolisi wa kinondoni na kusababisha kifo cha mtoto mdogo aliyepakiwa kwenye pikipiki huku watu watano wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali hizo huku ajali 5 zikiwa zimetokea kwenye mkoa wa kipolisi wa ilala na kusababisha majeruhi ya watu 05 pia.

Kamanda Mpinga amesisitiza kuwa hatua kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya madereva wasiofata sheria na kwamba hakutakuwa na fini kwa atakayekamatwa bali watafikishwa mahakamani na kupigwa picha na kuwekwa majina ya utambulisho,kosa,umri,na maeneo wanakotoka kisha kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ili kuepuka adha hiyo madereva wote wanatakiwa kuwa makini barabarani na kuacha kupita kwenye barabara ya magari yaendayo kasi  na ieleweke kuwa barabara hiyo ni maalumu kwa mabasi hayo tu na si vinginevyo amesema kamanda Mpinga.

 

 

 

 

 

 

 

 

Hizi ndizo tuhuma zinazomkabili Zitto Kabwe
Video: Zitto Kabwe Kaongea Haya Baada ya Mahojiano na Polisi