Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema itakuwa vigumu kumuacha Jamie Vardy nje ya kikosi chake cha Euro 2016 iwapo mshambuliaji huyo wa Leicester ataendeleza makali yake ya sasa.

Vardy alivunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy iliyodumu miaka 12 kwa kufunga mechi 11 mfululizo Ligi ya Premia.

Vardy, 28, amefungia Leicester mabao 14 msimu huu na amechezea Uingereza mara tatu.

“Hatafunga katika kila mechi kati ya sasa na wakati nitakuwa nikichagua timu. Lakini anaweza kuendelea kuwa Jamie Vardy, na kucheza kama Jamie Vardy,” amesema Hodgson.

Vardy, anaongoza ufungaji mabao Ligi ya Premia na amesaidia kufikisha Leicester kileleni kwenye jedwali.

UEFA Kuchezesha Droo Ya Champions League Leo
Nape awashauri Wanafunzi Vyuo Vikuu Kutumbua Majipu, Anusuru Mdahalo wa Hotuba ya Rais