Beki wa FC Barcelona Gerard Piqué Bernabéu, ameeleza umuhimu wa mchezo wa El Clasico, kwa kusema una umuhimu mkubwa kwao tofauti na ilivyo kwa Real Madrid.

Real Madrid wataelekea Nou Camp mwishoni mwa juma hili huku wakijivunia hatua ya kukaa kileleni kwa tofauti ya point sita dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona.

Pique, amesema umuhimu wa mchezo huo kwao ni kutaka kurejesha matumaini ya ushindani katika ligi hiyo, huku akiamini kwa wapinzani wao watahitaji kuukimbia ushindani kwa kutaka kupepea zaidi kileleni.

Amesema endapo itatokea wanaibuka na ushindi dhidi ya Real Madrid, watakua wamepunguza pengo la point tatu, ambalo litawasaidia kuwa kwenye mkakati mzuri wa kutetea ubingwa wa Hispania.

Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ametoa angalizo kwa mashabiki wa soka duniani kote kuamini kuwa, soka ni mchezo wa kupambana uwanjani na sio kuzungumzwa mdomoni kama ilivyo sasa, ambapo asilimia kubwa wanaamini kuna nafasi finyu kwa Barca kuibuka na point tatu.

“Kila mmoja wetu anatakia kuheshimu mchezo wa El Clasico na sio kuuona kama una umuhimu kwa upande mmoja kwa kigezo cha kuwa na point nyingi dhidi ya mwingine,” Alisema pique alipozungumza na gazeti la Mundo Deportivo.

“Kila mmoja anaweza kuibuka mshindi, lakini naamini kwetu itakua ni mchezo wenye umuhimu zaidi, kutokana na hitaji la kutaka kuendelea kuwa katika ushidani wa kuwania ubingwa, japo ninakiri upinzani utakua mkubwa.” Aliongeza beki huyo.

Possi aitaka jamii kuwa kwamua wenye ulemavu
Virgil van Dijk Kuziba Pengo La John Stones