Mahakama nchini Bangladesh, imewahukumu kifo watu 16 walioshiriki kumchoma moto hadi kufa mwanafunzi Nasrat Jahan Rafi (19) kwa kuripoti kuwa mwalimu mkuu amemnyanyasa kingono.
Nasrat alfariki mwezi Aprili katika mji wa Feni, uliopo kilomita 160 nje ya mji mkuu wa Dhaka, kifo chake kilishangaza wengi nchini humo na kupelekea msururu wa maandamano kushinikiza haki itendeke.
Miongoni mwa walio hukumiwa kifo ni mwalimu kuu aliyetuhumiwa kwa unyanyasaji na wanafunzi wawili wa kik, lakini Mawakili wa washtakiwa wanasema watakata rufaa.
Kesi hiyo ni ya kwanza kuamuliwa haraka nchini humo ikilinganishwa na nyingine kama hizo ambazo huchukua miaka kadhaa kabla ya kuamuliwa. Mwendesha mashtaka Hafez Ahmed aliwaambia wanahabari kuwa “wauaji sharti wachukuliwe hatua.
Uchunguzi wa mauaji ya Nusrat ulionesha njama ya kutaka kumnyamazisha ambayo pia ilihusisha wanafunzi katika darasa lake pamoja na wanaume walio na ushawishi mkubwa katika jamii.
Maofisa kadhaa wa polisi pia walipatikana na hatia ya kushirikiana na wale waliokamatwa kueneza taarifa za uwongo kwamba Nusrat alijitoa uhai, Wengine wawili waliopatikana na hatia ni Ruhul Amin na Maksud Alam, kiongozi wa chama tawala cha Awami League party.
Familia ya Nusrat, ambayo iliunga mkono hatua yake kwenda polisi mwezi machi, imepewa ulinzi.
Ikumbukwe kuwa Kwamujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, akidai mmoja wa marafiki zake alikuwa amechapwa.
Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu.
Alipokataa ndipo walipommwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto.
Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa “walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe “.
mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada ya kutoroka eneo la tukio, aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.
” Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chini kwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika pale na ndio maana kichwa chake hakikuungua ,” Bwana Majumder aliiambia BBC.
Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu asilimia 80% ya mwili wake ulikuwa na majeraha. Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka.
Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao.
Unyanyasaji wa kingono umekithiri sana nchini Bangladeshi kwani ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika misaada la ActionAid mapema mwaka huu ilibaini kuwa 80% ya wanawake wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza nguo huenda wamekumbana na visa vya unyanyasaji wakiwa kazini au kudhulumiwa kingono.