Mwimbaji Hussein Rashid maarufu kama Hussein Machozi ametangaza kuacha muziki na kuanza maisha mapya ya kawaida.

Hussein Machozi ambaye amewahi kutamba na ngoma kama ‘Utaipenda’, ‘Full Shangwe’ na ‘Kwa ajili Yako’ ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kutoona matunda anayoyatarajia.

Hussein Machozi 2

“Kubwa ambalo nataka niwasimulie Watanzania ambalo ninalo leo hii kwamba very soon ntaachia ngoma yangu mpya na ni ya mwisho kabisa kwa Hussein Machozi, namaanisha naacha muziki, naacha Bongo fleva nakuwa mtu wa kawaida raia wa kawaida ambaye nitaishi maisha yangu ya kawaida,” alisema Hussein Machozi.

Alisema kuwa hivi sasa ameamua kuelekeza nguvu zake kwenye shughuli ambayo anaamini anaimudu zaidi na inaweza kumbadilishia maisha yake kwa muda mfupi.

Hata hivyo, mwimbaji huyo alieleza kuumizwa na uamuzi aliouchukua kwa kuwa anaamini watanzania bado wanapenda kusikia muziki wake.

Asiyekubalika Na Wengi Aivusha Arsenal Barani Ulaya
Mkuu Wa Wilaya Aagiza Atakayeugua Kipindupindu Akamatwe, Ashtakiwe