Wakati serikali ikiendelea na jitihada mbalimbali zakukomesha ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuhamasisha usafi kwa vitendo, mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima ameagiza atakayeugua ugonjwa huo ashitakiwe.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo jana ikiwa ni siku maalum ya usafi kitaifa katika kuadhimisha siku ya uhuru, ambapo alidai kuwa kitendo cha kuugua ugojwa huo ni kinyume na taratibu za afya.

“Mtu yeyote atakayeugua kipindupindu katika Wilaya ya Mpanda, atatibiwa na baada ya kupona atakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka taratibu za afya. Lazima akamatwe kwa sababu kipindupindu kinasababishwa na uchafu,” alisema Mwamlima.

Alisema kuwa amechukua hatua hiyo kwa kuwa suala la usafi wa mazingira ni wajibu wa kila mwananchi na kwamba yeyote akakayewajibika na kuchukia uchafu ataepuka magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kipindupindu.

Chanzo: Mtanzania

Hussein Machozi: Nimeacha Muziki rasmi
Lowassa: Magufuli Anatekeleza Hoja Zangu na Chadema