Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni.

Lowassa aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu Seya) na mwanae.

“Haya mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema Lowassa.

Kauli hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo, majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.

 

Mkuu Wa Wilaya Aagiza Atakayeugua Kipindupindu Akamatwe, Ashtakiwe
Kikwete Ajibu Tuhuma Za Kulea Ufisadi Bandarini, Awapiga Kijembe Ukawa