Rais wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete jana aliungana na wananchi wa kijiji cha Msoga katika zoezi la kufanya usafi kama ilivyoagizwa na rais John Magufuli, ambapo alitumia nafasi hiyo kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Jakya Kikwete M

Dk. Kikwete amekanusha kuhusika kwa namna yoyote ile kuruhusu baadhi ya wafanyabiashara kupitisha makontena bandarini bila kulipa kodi.

Majibu ya rais huyo mstaafu yanakuja baada ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa Dk. John Magufuli kubaini makontena 349 yaliyopita bandarini bila kulipa kodi na kuchukua hatua ya kuwasimamisha kazi watendaji wa bandari hiyo na kuvunja bodi yake.

“Sijawahi wakati wangu kuagiza mtu yeyote asamehewe kontena lake lisilipe ushuru. Ningefanya biashara hiyo tusingefika bilioni 900,” alisema Dk. Kikwete.

Aidha, alirusha kijembe kwa kambi ya upinzani inayounda Ukawa ingawa hakuwataja.

“Wamekaa wanachonga tu, wale wanasumbuka bure. Wasinilaumu mie, Magufuli ndio kawashinda. Mgombea mzuri, wananchi wanamkubali, sasa wao wana kisa na mie,” alisema.

Dk. Kikwete aliwataka wananchi kumuunga mkono rais Magufuli katika jitihada za kupambana na ufisadi alizozianza kwa kasi.

 

Lowassa: Magufuli Anatekeleza Hoja Zangu na Chadema
BAKWATA yamtungua mkurugenzi wake, Ni Sakata la Kadhia ya Magari 82 na misamaha ya kodi