Kwa mara ya kwanza, Tanzania imepata muwakilishi kwenye tuzo kubwa na zenye heshima ya kipekee duniani, Tuzo za Grammy.

Allan Kingdom, ni rapa mwenye asili ya Tanzania aishie Marekani ambaye ametajwa kuwania tuzo za Grammy 2016 katiak vipengele viwili. Rapa huyo mwenye uwezo wa kipekee ameshirikishwa na Kanye West kwenye album yake ya mwaka huu ‘So Help Me God’.

Wimbo wake wa Áll Day’umemuwezesha kutajwa kwenye katika vipengele vya Best Performance na Best Rap Song zinazopatikana kwenye album yake ya Ep Nne.

Mama wa rapa huyo ni Mtanzania wakati baba yake ni raia wa Afrika Kusini. Rapa huyo alizaliwa nchini Canada kabla ya wazazi wake kuhamia nchini Marekani.

Mwadui FC Yadhihirisha Stand Utd Si Lolote Kwao
Lipumba aendelea kumngángánia Muhongo, Aibuka na Lingine