Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa na tabia ya kuwahurumia wajane na Yatima katika jamii yetu,huku akieleza kuwa idadi ya wajane inaongezeka kwa kasi kubwa mno katika jamii.

Alhaj Dk.Mwinyi ameyasema hayo mara baada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi hapo jana Mei 19, 2023.

Aidha, Ahaji Dkt. Mwinyi pia amewaomba waumini hao kuendelea kuwaombea dua za kheri viongozi wao, ili waweze kuiongoza vyema Zanzibar.

Katika hotuba yake ya Ijumaa Mei 12, 2023, Alhaj Dkt. Mwinyi pia aliwasisitiza waumini kuzingatia maadili ya dini na kushiriki kikamilifu shughuli za misikiti ikiwa kutumia misikiti kama vituo vya ibada na kujitolea katika kusaidia kuboresha na kudumisha misikiti hiyo.

Watendaji Wizara ya Elimu watakiwa kujitathmini
Mpango mkakati wa elimu ya Mazingira waiva