Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari Polisi kuhakikisha wanachukua hatua madhubuti za kudhibiti uhalifu na wahalifu hasa kwenye maeneo yao ya utendaji wa kazi hatua ambayo itasaidia Jeshi hilo katika kudhibiti vitendo hivyo.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara katika Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo amesema kuwa, kamwe hato furahia kuona askari Polisi akishindwa kudhibiti uhalifu na wahalifu na kuwafanya Watanzania wasiishi kwa amani na utulivu.

Wakati huo huo IGP SIRRO amekagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shule ya Polisi Moshi, ikiwemo ufugaji wa mifugo na kilimo cha mazao mbalimbali katika kujiongezea kipata na kupunguza gharama za uendeshaji wa shunghuli mbalimbali za shule hiyo.

Jeshi la Polisi latoa tahadhari
Wasafi wa kwaa kisiki kingine