Imefahamika kuwa kiungo kutoka nchini Ghana Thomas Partey amejiunga na Washika Bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal FC), kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 110.

Kungo huyo alikamilisha usajili wa kujiunga na Arsenal usiku wa kuamkia jana, na makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba The Gunners watailipa ada hiyo kwa awamu ndani ya miaka minne.

Arsenal ilitangaza kumsajili Partey kwa ada ya Pauni milioni 45, ambazo zilihitajika kuvunja mkataba wake na Atletico Madrid ya Hispania, lakini taarifa zilizoibuka baadae zimedai kuwa itaigharimu klabu hiyo ya London Pauni milioni 110 katika kipindi chote ambacho kiungo huyo atakaa Emirates Stadium.

Arsenal kwanza imelipa Pauni milioni 2.5 ada ya usajili, pia itamlipa Partey mshahara wa Pauni 260,000 kwa juma, jambo linalofanya saini yake kwa miaka minne kuwagharimu Pauni 110 milioni.

Saratani ya matiti tishio kwa wanawake
Young African, Simba SC wafunguka mabadiliko ya ratiba