Ritha Justin ni binti mdogo aliyekubwa na ugonjwa wa ajabu uliokatisha hadi masomo yake akiwa kidato cha pili, amepatwa na ugonjwa huo ambao hadi sasa amezunguka karibia kila sehemu na kukosa msaada.

Kila siku zinavyozidi kwenda Ritha anazidi kuwa na hali mbaya kwani hadi sasa hawezi hata kutembea pia kuongea ni kwa shida sana, wala hasikii.

Mama yeke Ritha, Jackline Menyee ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam akiisimulia MKASA ya Dar24 kuhusu binti yake, ameeleza kuwa amejaribu kwa kila njia kumsaidia Ritha lakini ameshindwa na hali ya binti yake inazidi kuwa mbaya kila siku zinavyozidi kwenda, hivyo ameamua kupaza sauti kuiomba Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amsaidie na kuokoa maisha ya mtoto wake mwenye ndoto kubwa iliyokatishwa na ugonjwa huo.

Kwa kweli anahitaji msaada wetu sote ili kumuokoa katika mkasa huu wa ajabu, mimi na wewe tunaweza kuwa sehemu ya maisha mapya ya furaha kwa Ritha, kwa kujitoa na kumsaidia kwa kile kidogo tunachoweza. Bofya hapa kutazama hapa MKASA huo

Korea Kaskazini yatoboa siri dhidi ya mpango wake wa nyuklia
Kizimbani kwa kujifanya mwanamke