Malaysia, msichana mwenye umri wa miaka 16, ameripotiwa kufariki dunia kwa kujiua baada ya kuweka posti kwenye mtadao wake wa istagram akiuliza aendelee kuishi au afe na asilimia 69 ya waliojibu swali hilo walimtaka afe huku asilimia 31 wakimtaka aishi.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa kifo hiko cha binti ambaye jina lake bado halijafahamika ambaye aliweka post hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa istagram na kuandika;
”Muhimu sana, nisaidie kuchagua, niishi au nife” ambapo asilimia kubwa ya watu waliojibu ujumbe huo walichagua afe na ndipo aliamua kuchukua uhai wake.
Ramkarpal Singh, mwanasheria na Mbunge wa Kusini Mashariki mwa mji wa Penang amesema binti huyo angekuwa hai endapo wengi wao kwenye mtandao wa Instagram wangesema aishi.
Waziri wa michezo na vijana Malaysia, Syed Saddiq Syed Abdul Rahman amesema janga hilo lililotokea nchi linahitaji mazungumzo kwa jinsi gani wanaweza kuwasaidia vijana kutokana na msongo wa mawazo na amepata wasiwasi mkubwa juu ya mawazo ya vijana wengi nchini humo, amesema ni janga la taifa lazima lichukuliwe kwa makini zaidi.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Instagram, Ching Yee Wong amesema mawazo na sara zao ni juu ya wasichana wadogo, ameongezea kuwa ni jukumu lao kuhakikisha kuwa watu wanatumia na kuona mtandao wa istagram kama sehemu salama.