Waziri wa Utalii wa Israel Asaf Zamir amejiuzulu leo akipinga sheria mpya inayozuia maandamano dhidi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu.

Zamir ametangaza kujiuzulu kwake kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook akisema dhamira yake haimruhusu kuendelea kuhudumu katika serikali inayopinga maandamano na kwamba hana imani na kiongozi huyo.

Zamir ambaye anatokea chama cha samawati na nyeupe kinachoongozwa na mpinzani wa Netanyahu, Benny Gantz amesema Netanyahu anaiongoza Israel kulingana na malengo yake binafsi ya kisiasa.

Kwa miezi sasa, kumeshuhudiwa maandamano Israel dhidi ya Netanyahu kutokana na jinsi alivyovishughulikia virusi vya corona nchini humo na pia madai ya ufisadi yanayomkabili, jambo analopinga.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 3, 2020
Safari ya kwanza ya treni kutoka Dar - Arusha yazinduliwa