Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutimiza majukumu yao kikamilifu ili kuchochea maendeleo

Ameyasema hayo mapema hii leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na watumishi wa halmashauri hiyo, Jafo amesema kuwa endapo kila mtumishi akitimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii kero na matatizo yanayowakabili wananchi yatabaki kuwa historia

Aidha, Jafo amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara kuweka mipango ya uendeshaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo na kujitathmini kama wamefanikiwa kiasi gani na kama wamefeli wafanyaje ili makosa hayo yasijirudie.

Hata hivyo, Kwa upande wake Meya wa Halmashauri hiyo, Charles Kuyeko amepongeza jitihada zinazofanywa na Naibu Waziri huyo na kuahaidi wataendelea kuyafanyia kazi maagizo yake.

Video: Ziara ya JPM yaondoka na bosi Magereza, Sakata la Dangote lafichua siri nzito...
Video: Makonda afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi ofisi za bakwata