Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serkali za Mitaa, Selemani Jafo amesema uchaguzi wa Serikali za mitaa uko pale pale na utafanyika Novemba 24, 2019 kama ilivyopangwa licha ya vyama vingine kujitoa kwenye uchaguzi huo.
Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja kutoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi sambamba na kamati za rufaa.
Waziri Jafo amebainisha kuwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi limeenda vizuri na wananchi waliochukua fomu ni 555,036 na waliorejesha ni asilimia 2.7 tu.
Wizkid, Tiwa savege kwenye ardhi ya Tanzania
“Hii inaonesha muamko mkubwa wa wananchi kutaka kuongoza katika ngazi ya Serikali za mitaa na mchakato mzima wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ulienda vizuri ukiwa na kanuni bora zaidi kulingana na chaguzi zilizotangulia ” amesema Jafo.
Ameongeza kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika lilifuatiwa na uteuzi ambao ulilenga kuteua wagombea wenye sifa, waliokidhi vigezo na kufuata taratibu zote za ujazaji wa fomu za kugombea na kubandikwa kwa orodha ya wagombea waliopitishwa katika hatua hiyo.
CHAUMA waunga tela kususia uchaguzi
Wagombea pia walipata fursa ya kuwasilisha pingamizi zao kwa mujibu wa kanuni na kisha kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa za Wilaya zilizoundwa kwa ajili ya kuratibu rufaa za wagombea.
Waziri Jafo amefafanua kuwa mpaka sasa hivi rufaa zilizowasilishwa kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa ni 13,500 na zinafanyiwa kazi na kamati za rufaa za uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo zoezi hilo litakamilika leo Novemba 11, 2019.
Aidha amesisitiza kuwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, jina la mgombea likishateuliwa linabaki kwenye karatasi za kupigia kura hata kama chama chake kimejiengua kushiriki kwenye ushaguzi.